Tuesday, January 22, 2013

TAREHE 5.01.2013 TULITEMBELEA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO LA AMBONI LILILOPO HAPA TANGA MJINI

Ilikuwa ni jumamosi ya kwanza katika mwaka huu 2013, tulijumuika pamoja na washiriki wa kanisa la waadventista wa sabato amboni katika kumshukuru Mungu kwa ulinzi wake kwa mwaka mzima 2012. Tulishirikiana katika ibada tangu shule ya sabato hadi huduma kuu. 


Kwaya nzuri ya thisdaso alishiriki vyema katika kumtukuza Mungu wa mbinguni ikishirikiana kwa moyo wote na kwaya wenyeji wa kanisa la Amboni.


Siku hii ilikuwa maalum kwa kufunga na kuomba kwa ajili ya shukrani kwa mwenyezi Mungu na kumualika kutembea pamoja nasi na kutupatia roho wake mtakatifu ili atuongoze katika safari yetu kuelekea mbinguni, kwa sababu kwa hakika bila Roho wa Mungu ndani yetu hatutafanikiwa. 


Tulishiriki mibaraka pamoja na wenyeji kuanzia asubuhi hadi saa11:00 jioni tukiwa pale kanisani.

 

ZIFUATAZO NI BAADHI YA PICHA ZA MATUKIO YA SIKU HIYO.

 

 























No comments:

Post a Comment